Telnolojia bila kuwa umeelimika daima utakuwa unaona kuwa kuna kitu umepungukuiwa ili kuweza kufurahia ulimwengu wa kidijiti na pale utakafanya maamuzi ya kuitafuta elimu basi kuwa na kompyuta kwa ajili ya wanafunzi litakuwa suala la kawaida sana.
Ngamizi maarufu kama kompyuta lakini ukitaka kuzungumzia zile zinazobebeka kirahisi tunasema “Vipakatalishi” ambavyo vipo katika makundi mbalimbali mathalani zenye uwezo wa kawaida, kati na mkubwa zaidi.
Siku si nyingi zilizopita HP walizindua kompyuta mpakato mbili ambazo wameziunda kwa kulenga watu ambao wanasoma kwa lugha nyingine ni wanafunzi. Sasa kwanini ngamizi hizo zinawafaa zaidi wanafunzi? Kupata majibu tazama jedwali lifuatalo:-
Kipengele | HP Chromebook x360 11 G2 | HP Chromebook 11 G7 EE |
Kioo | Kioo kina urefu wa inchi 11 (1366 x 768px) IPS ambacho pia ni cha mguso | Kioo kina urefu wa inchi 11 lakini sio cha mguso katika matoleo mawili tofauti; IPS na SVA |
Muonekamo | Ina uwezo wa kuzungushwa mpaka nyuzi 360 na kuitumia kama tabiti | Inaweza kuzungushwa mpka nyuzi 180 pekee (haiwezi kutumika kama tabiti) |
Kipuri mama | Dual-core Celeron N4000ama quad-core N4100 | Dual-core Celeron N4000ama quad-core N4100 |
Kipengele | HP Chromebook x360 11 G2 | HP Chromebook 11 G7 EE |
RAM/Diski uhifadhi |
|
|
Betri |
Inakaa na chaji kwa muda wa saa 11.5
|
Inakaa na chaji kwa muda wa saa 13
|
Mengineyo |
|
|
Bei zake zinatarajiwa kufahamika hapo baadae lakini zitaingia sokoni mwezi Aprili 2019. Vipi vipakatalishi hivi umependezwa navyo?
from tekokona
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni